Benki ya dunia imetangaza msaada wenye thamani ya dola bilioni
57.wa miaka mitatu kwa mataifa yaliyoko kusini mwa jangwa la sahara huku sehemu
kubwa ya msaada huo utatumiwa katika kutoa dhamana kwa mikopo isiyo na riba kwa
baadhi ya mataifa maskini zaidi duniani .
Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim anasema udhamini huo wa
kifedha utayasaidia mataifa ya Afrika kuwa na ukuaji wa kiuchumi , kubuni
nafasi za ukuaji huo pamoja na kuyalinda dhidi ya hasara na mizozo ya kiuchumi
Kiwango cha pesa zenye thamani ya dola bilioni 45 kitatolewa kwa
mataifa hayo kupitia Jumuiya ya kimataifa ya Maendeleo, ikiwa ni kitengo cha
Benki ya dunia kinachohusika zaidi na mataifa maskini zaidi duniani .
Msaada huo wa fedha utasaidia
kuboresha miradi 400 inayoendelea katika mataifa yaliyoko chini ya jangwa la
sahara, kuanzia ile inayohusika na maendeleo ya miundo mbinu , elimu, utoaji wa
huduma ya maji safi na huduma za afya za msingi.
Lengo ni kubuni hali
itakayoweza kuinua uchumi na wachambuzi wanasema msaada huu kutoka benki ya
dunia, unaweza kusaidia kwa kiwango kikubwa kuimarika kwa mchakato wa kufufua
uchumi wa mataifa hayo
0 comments:
Post a Comment