Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetaja shule kumi bora ambazo zimeongozwa
na shule ya sekondari ya Feza Girls ya Dar es Salaam ambayo imeibuka kinara kwa
watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili, ikifuatiwa
na Marian Boys (Pwani) iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika
nafasi ya tatu na Ahmes (Pwani) imeshika nafasi ya nne. Marian Girls (Pwani)
iliyoshika nafasi ya tano, Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde
Juu (Tanga) nafasi ya saba, Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza Boys (Dar
es Salaam) nafasi ya tisa na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.
Orodha ya shule kumi
bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita
|
Shule zilizoshika mkia ni Kiembesamaki ya Unguja, Hagafilo (Njombe),
Chasasa (Pemba), Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam), Ben Bella (Unguja), Meta
(Mbeya), Mlima Mbeya (Mbeya), Al-Ihsan Girls (Unguja) na St Vicent(Tabora).
0 comments:
Post a Comment