Serikali ya awamu ya tano sasa
imeanza kutangaza nafasi za ajira kwenye vitengo mbalimbali baada ya kipindi
kirefu cha mpito kilichosababishwa na uhakiki wa watumishi hewa na wenye vyeti
vya kughushi.
Ongezeko kubwa la wahitumu
kuanzia ngazi ya cheti, stashahada na shahada limesababisha soko la ajira kuwa
gumu sana, lakini pamoja na ugumu huo bado kuna wahitimu wengi hawajui hatua
zinazopaswa kufuata wakati wa kuomba ajira.
Ikumbukwe kuwa kwa sasa
serikali inatumia mfumo wa kielektroniki (recruitment portal) kutangaza nafasi
za ajira na kufanyia maombi. Na yapo baadhi ya mabadiliko na mambo ya msingi ya
kuzingatia kabla ya kuomba nafasi zinazotangazwa na serikali kupitia utumishi.
Haya ni maelekezo juu ya hatua
zinazopaswa kufuatwa wakati wa kuomba nafasi za ajira kupitia ‘recruitment portal’
1. Muombaji anapaswa kuwa na
vyeti vinavyohitajika wakati wa kufanya maombi N.B. result slip, transcript na
affidavit havihitajiki kwenye mfumo huu.
2. Kama muombaji hana baruapepe
‘email’ unapaswa kufungua baruapepe
yake mwenyewe na uhifadhi namba/neno lake la siri (password)
3. Mwombaji atoa copy vyeti
vyote anavyohitaji kuvitumia wakati wa kufanya maombi Mfano: cheti cha shahada, academic
certificate ya kidato cha nne na cha sita; na cheti cha kuzaliwa.
4. Muombaji apige picha
(passport size) kisha achukua ‘soft copy’
yake na kuihifadhi kwenye vifaa maalum vya kutunza kumbukumbu Mfano: kwenye
flash, simu, laptop nk
5. Muombaji atatakiwa kuchukua
vyeti vyako pamoja na nakala zake (copy) kisha apeleka kwa wakili au mahakamani
kwa ajili ya kuhakikiwa na kugongwa muhuri wa kuthibitisha uhalali wa vyeti
vyake.
6. Mwombaji achukue nakala
zake za vyeti zilizogongwa muhuri wa wakili au mahakama na aviscani ilia pate ‘PDF’.
Pia ahakikishe kila cheti kinakaa kwenye kumbukumbu yaake na kukipa jina
linalotofautisha cheti hiko na kingine. Mfano: cheti cha kidato cha nne utakipa
jina ‘form four’, cheti cha kidato
cha sita unakipa jina ‘form Six’ n.k
7. Muombaji achukue ‘soft copy’
ya vyeti alivyo’scan’ pamoja na ‘soft copy’ ya picha ndogo ‘passport size’ aliyopiga
mwanzoni kisha ahifadhi kwenye faili moja ili kurahisisha upatikanaji wa
taarifa wakati wa ku’upload’.
8. Muombaji aingie kwenye
tovuti ya utumishi www.ajira.go.tz kisha aenda sehemu ya ‘recruitment portal’
halafu aingie kwa kutumia baruapepe yake aaliyoifungua hapo awali na neno/namba
ya siri. Hapo muombaji aanze kujisajili kama mwanachama mpya. Aingize email
yake na ataweka ‘password’ kisha utaanza kuingiza taarifa zako kama zinavyojionesha
kwenye website. Mfano: taarifa binafsi, taarifa za taaluma, taarifa za ajira n.k.
9. Muombaji afahamu kuwa kila
sehemu inayohitaji cheti hususani sehemu ya taaluma ahakikishe ame’upload’
cheti chake husika, na akimaliza hatua hizo, ukurasa ‘profile’ yake itaonesha
siyo chini ya 90% kama muombaji amejaza vizuri taarifa zako na kuweka vyeti
vyake.
Baada ya kumaliza haua hizo
muombaji anakuwa tayari kwa kuomba nafasi za ajira zilizotangazwa kwenye tovuti
hiyo kulingana na taaluma yako.
10. Namna ya kuomba, muombaji aandike
barua ya maombi ya ajira kisha a’upload’ kwenye tangazo husika.
Hapo muombaji atakuwa tayari amemaliza
kufanya maombi yake ya ajira, tayari kwa kuhudhuria usaili endapo muombaji
atakua ametimiza vigezo vya kuitwa.
a signed application letter, hapa sijaelewa, yaan una isaini kwenye hard copy halafu unahiscan na kuiupload au vip? msaada tafadhali
ReplyDeleteWebsite ya utumishi inasumbua. baadhi ya vipengele avifunguki asa kwenye kipengele cha elimu
ReplyDeleteKwaiyo kama sijapata cheti siwezi kutumia transcript kuomba kazi?
ReplyDeleteMi sijaelewa passport size unaiatach sehem gani
ReplyDelete