Wanafunzi saba wamefariki na
wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya moto kuchoma bweni la shule ya Moi Girls
mjini Nairobi nchini Kenya. Waziri wa elimu nchini Kenya Fred Matiang'i amesema
kuwa wanafunzi kumi waliojeruhiwa wamelazwa hospitalini huku wawili kati yao
wakiwa na hali mbaya.
Baadhi ya Majengo ya Shule ya Moi Girls yakiwa
yanaungua kwa moto
|
Maafisa wa habari wa shirika
la msalaba mwekundu katika shule ya Moi Girls wameeleza kuwa takriban wanafunzi
kumi hawajulikani waliko kufuatia tukio hilo Naye waziri Matiang'i amesema kuwa
shule hiyo imefungwa kwa muda wa wiki mbili kupisha uchunguzi kuhusiana na
sababu ya moto huo.
Waziri huyo ameeleza kuwa
wanafunzi wa kidato cha nne wataendelea na masomo yao ifikiapo siku ya Ijumaa
na watasaidiwa kuendelea na masomo yao wakati ambapo wanajianda kufanya mtihani
wa kidato cha nne wa KCSE. Mkuu wa shule hiyo amewataka wazazi kuwachukua
wanawao.
Kulingana na gazeti la Daily
Nation nchini humo mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza ambaye alikuwa
miongoni mwa wale waliotibiwa baada ya kisa hicho alisema kuwa moto huo ulianza
mwendo wa saa saba usiku.
Alisema kuwa bweni
lililochomeka lilikuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza na kwamba kulikuwa na
makelele ya wanafunzi waliojaribu kujinusuru mbalii na mkanyagano huku
wasichana wakijaribu kuAlisema kuwa bweni lililochomeka lilikuwa na wanafunzi
wa kidato cha kwanza na kwamba kulikuwa na makelele ya wanafunzi waliojaribu
kujinusuru mbalii na mkanyagano huku wasichana wakijaribu kutoka ndani ya bweni
hilotoka ndani ya bweni hilo
0 comments:
Post a Comment