Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini Tanzania (HESLB) imetoa vigezo na sifa kwa
waombaji wa mikopo ya elimu ya juu na kuainisha ni wapi hasa wanastahili kupata
mikopo hiyo kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa, ambapo watoto wa vigogo
kutotarajiwa kuomba mikopo hiyo.
Bodi
hiyo ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Agosti 6 imeanza
kupokea maombi ya mikopo ambapo mwisho wa uombaji wa mikopo hiyo unatarajiwa
kuwa tarehe 4 Septemba, 2017.
Bodi hiyo imetoa vigezo kumi vya msingi kwa waombaji wa mikopo ya elimu ya juu, ambavyo ni;
- Mwombaji awe Mtanzania
- Mwombaji awe ameomba
kudahiliwa na chuo kikuu au taasisi ya elimu ya juu inayotambuliwa na
serikali
- Asiwe mwanafunzi wa masomo
ya jioni
- Asiwe na
udhamini/ufadhili/msaada wa kifedha kutoka katika vyanzo vingine
- Awe ameomba mkopo kupitia
mfumo wa mtandao (OLAMS)
- Awe amefaulu mitihani ya
mwisho wa mwaka (kwa wanaoendelea na masomo) na matokeo yake kuwasilishwa
bodi ya mikopo na chuo chake
- Awe amemaliza kidato cha
sita au awe na sifa linganishi (kama Diploma n.k) ndani ya miaka
(2015/12-2017/18)
- Awe na umri usiozidi miaka
30 wakati wa kufanya maombi
- Waombaji ambao wazazi wao ni
wakurugenzi au mameneja waandamizi katika makampuni binafsi
yanayotambuliwa na mamlaka za mapato na usajili hawatarajiwi kuomba
- Waombaji ambao wazazi wao ni
viongozi wa umma au kisiasa ambao wanatajwa na sharia ya maadili ya
viongozi wa umma hawatarajiwi kuomba mikopo
0 comments:
Post a Comment