Rais wa
Afrika kusini Jacob Zuma ameponea chupuchupu kung’olewa kwenye kiti cha urais
kufuatia kura ya kutokuwa na imani naye zilizopigwa bungeni leo baada ya
wabunge wengi wa chama tawala cha ANC kumuunga mkono.
Rais Jacob Zuma |
Jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa ni
384, wabunge 177 walipiga kura ya kumuondoa madarakani rais Zuma kwa kutokuwa
na Imani naye, wabunge 198 walipiga kura ya kumuunga mkono huku jumla ya kura
tisa zikiharibika.
Wafuasi wa rais Jacob Zuma
walishangilia ushindi huo kupitia vigelegele na kucheza densi. Hata hivyo wabunge
40 wa chama tawala cha ANC walipiga kura ya kutaka kumng'atua mamlakani
kulingana na mwandishi wa BBC Milton Nkosi kupitia ujumbe wake wa Twitter.
Chama cha upinzani nchini humo
Democratic Alliance kinasema kuwa wabunge wengi wa chama tawala cha ANC
walipiga kura hiyo wakizingatia maswala ya ufisadi.
Lakini ushindi wake ulikuwa mdogo ,
ikimaanisha kwamba idadi kubwa ya wabunge kutoka chama tawala cha ANC iliunga
mkono muswada huo wa upinzani kumuondoa madarakani.
Kura hiyo ya kutokuwa na Imani na
Rais Zuma inapigwa mara ya nane sasa tangu rais huyo aingie madarakani huku
msukumo mkubwa ukitoka kwa waandamanaji na vyama vya upinzani vinavyotaka Rais
huyo ang’atuke kwa kile kinachodaiwa kukithiri kwa vitendo vya kifisadi
vinavyofanywa na Rais huyo na seikali yake.
0 comments:
Post a Comment