Serikali ya Zimbabwe imetenga
jumla ya Dola za kimarekani Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha
kumbukumbu cha Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe
kwa ajili ya utafiti na uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia ambacho
kinatarajiwa kujengwa mjini Mazowe.
![]() |
Rais Robert Mugabe |
Akizungumza na waandishi wa
habari leo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Jonathan Moyo amesema
Chuo Kikuu cha Robert Gabriel Mugabe kitakuwa chuo cha kwanza kwa kuwa na
miundombinu kwa ajili ya masomo ya sayansi, uhandisi na teknolojia kwa asilimia
mia moja.
“Wizara imeridhika na maamuzi
ya serikali kuanzisha Chuo kikuu cha Robert Mugabe, hautotambulika uwajibikaji
wa Rais Mugabe kwenye elimu” amesema waziri Jonathan
“Tunapanga kufanya kazi pamoja
na taasisi ya Mugabe Foundation na Chuo Kikuu cha Zimbabwe kuanzisha Chuo cha
Robert Gabriel Mugabe, kitakuwa chuo kitakachowezesha uvumbuzi wa kisayansi,
kiuhandisi na kiteknolojia ili kuboresha hali ya maisha” amesema Waziri
Jonathan
Mamlaka yenye jukumu la
kusimamia uanzishwaji wa Chuo kikuu cha Robert Gabriel Mugabe ni Taasisi ya Mugabe
Foundation ambayo wadhamini wake wakuu ni Rais Mugabe na mke wake Dr. Grace
Mugabe
0 comments:
Post a Comment