UCHAGUZI MKUU KENYA, ULIVYOGUBIKWA NA MATUKIO WAKATI WA UPIGAJI KURA

Raia wa Kenya wameshiriki oezi la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017 jana tarehe 8 Agosti, ambapo kwa mwaka huu yapo matukio ambayo hayajawahi kutokea mara kadhaa katika chaguzi kuu nchini humo. Matukio hayo yameibua hisia na maoni tofauti kwa watu nchini humo ambapo wafungwa, na wagonjwa mahututi pia walishiriki zoezi hilo.

Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Patrick Atindo mwenye umri wa miaka 64 alifariki dunia baada ya kupiga kura katika kituo ch Sule ya msingi Lela kaunti ya Kisumu, ambapo kabla ya mauti Patrick alikimbizwa hospitali siku moja kabla baada ya kulalamika maumivu ya kifua.
Mtoto wake Silvanus Ouma alisema baba yake aliamka saa 11 asubuhi tayari kushiriki zoezi la kupiga kura na aliondoka nyumbani akiambatana na mkewe Mary Atinda.
Tukio lingine ni lile la wagonjwa ambao walikuwa mahututi kutolewa mahospitalini na kupelekwa kwenye vituo vya kupigia kura, ambapo mwanaume mmoja alifikishwa katika kituo cha kupigia kura akiwa na mashine ya kupumulia kwa kutumia gesi.
Mwanaume aliyefahamika kwa jina la John Nyakundi mwenye umri wa miaka 53 katika kituo cha kupigia kura ha Shule ya Msingi ya Dandora alifikishwa kwenye kituo hiko cha kupigia kura akiwa na mtungi wa gesi kwa lengo la kupiga kura
Wagonjwa wengine wengi wao wakiwa waliolazwa katika jimbo la uchaguzi la Runyenjes, huku wengine wakionekana na mabandeji makubwa na dripu, wagonjwa hao walipewa kipaumbele cha kupiga kura.
Huko katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Mseto ya Sekondari Konyau alijifungua baada ya kusimama kwenye foleni kwa Zaidi ya masaa matatu. Imeelezwa na Diwani wa kata ya Kapchok anayemaliza uda wake kuwa mwanamke huyo alihisi uchungu akiwa kweny foleni huku akikataa kuwahishwa hospitali kabla ya kupiga kura.
Mwanamke mwingine mwenye umri wa miaka 33 alijikuta mimba ikitoka akiwa kwenye foleni katika kituo cha kupigia kura cha Kuwit baada ya kuhisi uchungu wa kuzaa huku akiwa na joto kali.
Katika tukio linguine mke wa Uhuru Kenya alikaa kwenye foleni kwa saa nne ili kupiga kura.
Kwa mara ya kwanza nchini Kenya wafungwa walipata nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu mwaka huu 2017. Katika gereza lenye ulinzi mkali la Kamiti, mkuu wa timu ya usimamizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Africa Thabo Mbeki alieleza kuwa tukio hilo ni hatua kubwa inayoleta matumaini kwa wafungwa kuwa nao wanaweza kuwa mchango kwa jamii
Kijana aliyejitolea usafiri kwa wanawake wajawazito, wazee na vipofu  kuwafikisha vituo vya kupiga kura

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment