CCM IMEWATEUA MAKATIBU WAPYA WA MIKOA NA WILAYA


Chama Cha Mapinduzi CCM kimefanya uteuzi wa makatobi wa mikoa 31 na makatibu wa wilaya 25. Orodha hiyo imetajwa leo na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hiko Mhe. Humphrey Polepole katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ndogo za chama hiko Lumumba mjini Dar es salaam. Uteuzi huo umefuata mara baada ya siku kadhaa ambapo chama hiko kiliwafuta uanachama baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya ikiwemo makatibu.


Makatibu wa Mikoa wakioteuliwa ni;
Arusha - Elias Mpanda
Dar - Saad Kusilawe
Dodoma - Jamila Yusuf
Geita - Adam Ngalawa
Iringa - Christopher Magala
Kagera- Rahel Degeleke
Katavi- Kajoro Vyahoroka
Kigoma- Naomi Kapambala
Kilimanjaro- Jonathan Mabihya
Lindi-Mwanamasoud Pazi
Manyara -Paza Mwamlima
Mara -Innocent Nanzabar
Mbeya -Wilson Nkhambaku
Morogoro- Kulwa Milonge
Mtwara -Zacharia Mwansasu
Mwanza- Raymond Mwangala
Njombe- Hossea Mpagike
Pwani- Anastanzia Amasi
Rukwa- Loth Ole Nesere
Ruvuma- Amina Imbo
Shinyanga -Haula Kachambwa
Simiyu- Donald Etamya
Singida- Jimson Mhagama
Tabora- Janeth Kayanda
Tanga- Allan Kingazi.
Ambapo kati ya makatibu hao 31 wa mikoa, makatibu 20 ni wapya

Makatibu wapya wa mikoa wa CCM ni;
Hanafi Msabaha- Kinondoni
Robert Kelenge- Kigamboni
Martin Mwakitabu- Chamwino
Asia Mohameh Chemba
Nuru Ngeleja- Chato
Clemence Mponzi- Kilolo
Mohamed Mfaume Bukoba Mjini
Mwajuma Boha- Misenyi
Miriam Kaaya- Moshi Vijijini
Agness Msuya- Siha
Mayasa Ayoub- Kilwa
Rafael Maumba- Liwale
Othman Dunga- Hanang
Rehema Ndele- Mbozi
Shaibu Mtawa- Morogoro Vijijini
Alfred Mwambeleko- Masasa
Said Mkoa- Sengerema

Mbali na hilo katibu wa itikadi na uenezi wa CCM pia alilizungumzia suala la RC Makonda na kusem suala hilo ni la kiuteuzi ni la rais pekee, anapomteua mtu anaweza pia kumchukulia hatua. Aliongeza kwa kusema chama kitakapokuwa tayari kitalishughulikia hilo suala. 
"Mkuu wa mkoa ni mteule wa Rais na anapomteua anamteua yeye peke yake na halazimiki kushauriana na mtu” alisema Polepole. 

Polepole pia aliongezea kwa kusem a mabadiliko ya katiba ya chama hiko yaliyofanywa hayahusu kipengele cha mchakato wa kumpata mgombea wa urais katika chaguzi za mwaka 2020
“Hakuna sehemu yoyote ya mabadiliko ya katiba tuliyoyafanya yanayohusu mchakato wa kumpata mgombea wa urais wa uchaguzi wa mwaka 2020” alisema Polepole
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment