Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete
pamoja na madiwani wa halmashauri ya Chalinze ,wameujia juu uongozi wa Mamlaka
ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Chalinze CHALIWASA kwa kushindwa kusambaza
maji ili kuondoa kero hiyo. Amesema mradi huo ulitakiwa kukabidhiwa mwezi huu jimboni hapo
lakini unasuasua.
Ridhiwani aliyasema hayo kwenye baraza la
Madiwani lililofanyika Lugoba.
Alisema tatizo la ukosefu wa maji, bado ni
kubwa hivyo inaonekana uongozi wa Mamlaka hiyo umeshindwa kutatua. Ridhiwani alifafanua kwamba
hadi sasa hakuna matenki yaliyojengwa na mabomba hayajafukiwa hivyo ni ndoto za
alinacha mradi huo kukamilika mwezi huu.
Kwa mujibu wake, waziri wa maji anapaswa
kulieleza bunge na wananchi wa Chalinze fedha za maji zilizopelekwa kwa ajili
ya mradi huo na mwezi wa kuumaliza. "Kama mradi huu utaendelea kusuasua wananchi na wawekezaji
wanaokimbilia kuwekeza Chalinze watashindwa kutimiza malengo yao na kuendelea
kuishi kwenye adha hii inayowapa wakati mgumu" alisema Ridhiwani.
Nao madiwani walisema, kama uongozi wa mamlaka
hiyo umeshindwa kazi basi wawapishe. Diwani wa Lugoba, Rehema Mwene,aliiomba serikali imsimamie mjenzi
wa mabomba na matenki amalize kazi hiyo.
Nae Hassan Mwinyikondo, alieleza hatari kubwa
kwa wananchi wa maeneo ya Bwilingu na Chalinze ambao wanatumia maji yasiyo safi
wala salama. Alisema mradi wa maji wa CHALIWASA hauna faida, kutokana na
wananchi kukosa maji kwa kipindi kirefu.
Hussein Hading'oka aliweka hofu katika kipindi
kinachokuja kuwa cha mvua za masika na kuongeza kwamba mara kadhaa viongozi wa
CHALIWASA wamekuwa wakisema kipindi cha mvua mitambo yao huwa inasumbuliwa na
tope hivyo kushindwa kufanyakazi za kusukuma maji.
Meneja wa Mamlaka hiyo Mhandisi Christer
Mchomba kushindwa kuhudhuria kikao hicho kama alivyotakiwa na Mkurugenzi Edes
Lukoa Meneja huyo alitakiwa kwa ajili ya kuwapatia Madiwani hao maelezo
ya kina kuhusiana na tatizo sugu la maji linalowakabili wananchi wa Halmashauri
hiyo kwa miaka mingi sasa. Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,
Edes Lukoa alisema Halmashauri imetenga bajeti iwa ajili ya maeneo ambayo
hayafikiwi na CHALIWASA hivyo mamlaka hiyo lazima iwe na mpango wake.
Hivi karibuni Waziri wa Mazingira Januari
Makamba alipofanya ziara ndani ya Halmashauri hiyo alifika eneo la chanzo cha
maji Wami na kutoa maagizo kwa wilaya na mkoa. Aliagiza Mkuu wa wilaya Alhaj Hemed Mwanga kuhakikisha na Mkoa
wanakutana na wenzao wa Morogoro kuzungumzia suala la wafugaji wanaotokea
Morogoro kuvamia kando ya mto WAMI na kuhakikisha wakulima wanaolima kando ya
mto wondolewe mara moja.
0 comments:
Post a Comment