POLISI 40 WAUAWA MJINI KASAI, DR CONGO


Umoja wa mataifa (UN) umesema watu 400 wameuawa tangu Agosti mwaka jana.
Wanamgambo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamewashambulia na kuwaua kwa kuwakatakata wanajeshi takriban 40 baada ya kuwavizia katika mkoa wa Kasai, katikati mwa nchi hiyo, maafisa wa serikali wamesema.
Wapiganaji hao kutoka kundi la Kamwina Nsapu walishambulia polisi waliokuwa kwenye msafara.
Maafisa sita wa pilisi waliowasiliana na Tshiluba waliachiliwa huru, rais wa bunge la jimbo la Kasai Francois Kalamba amesema. Machafuko jimbo la Kasai yalianza Agosti mwaka jana, pale maafisa wa polisi walipomuua kiongozi wa Kamwina Nsapu.
Gavana wa jimbo hilo Alexis Nkande Myopompa amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu mauaji hayo. Umoja wa Mataifa unasema watu 400 wameuawa na wengine 200,000 kuachwa bila makao eneo la Kasai tangu Jean-Pierre Pandi, kiongozi wa Kamwina Nsapu alipouawa.
Mauaji yake yalitekelezwa miezi miwili baada ya Kamwina Nsapu mwezi Juni 2016 kuanzisha juhudi za kutaka atambuliwe kama mkuu wa eneo hilo na kutaka maafisa wa serikali ya taifa kuondoka jimbo hilo.
DR Congo imekabiliwa na hali ya wasiwasi kisiasa huku Rais Joseph Kabila akiendelea kukaa madarakani kwa muda zaidi kuliko alivyoruhusiwa kikatiba Umoja wa Mataifa unasema umepata makaburi 10 ya pamoja ambapo waliouawa katika machafuko hayo walizikwa.
Kadhalika, kuna maeneo mengine saba ambapo inadhaniwa kuna makaburi yaliyozikwa watu wengi kwa pamoja.
Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa, Mmarekani na raia wa Sweden, walitekwa nyara eneo hilo wiki mbili zilizopita pamoja na raia wanne wa DR Congo waliokuwa wakifanya kazi nao ambapo mpaka kufikia sasa bado hawajulikani walipo.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment