Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma
(PIC) imeushauri uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC)
kuelekeza nguvu ya uwekezji katika mji wa Dodoma ili kuziba kukidhi ongezeko la
huduma za kumbi za kufanyia muikutano linalosababishwa na serikali kuhamia
katika mji huo.
Akizungumza katika kikao cha majumuisho baada ya
Kamati ya PIC kutembelea AICC mwishoni mwa wiki na kukagua miradi miwili,
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Albert Obama ameshauri AICC kuupa kipaumbele mkoa wa
Dodoma katika mkakati wa kujenga kituo kingine cha kisasa cha Mikutano.
“Tunahitaji kuiona taasisi hii ikipanuka na kujenga
vituo vingine vya mikutano huko mikoani na moja ya mikoa ambayo tungependa
muipe kipaumbele ni Dodoma maana huko ndio serikali inahamia na mahitaji ya
huduma ya kumbi za mikutano yanakwenda kuongezeka”, alisisitiza Obama.
Nae Mjumbe wa Kamati hiyo, Amina Mollel alieleza
kufurahishwa na juhudi za uongozi wa AICC kumilisha ujenzi wa mradi wa nyumba
za kisasa (apartment) 48 ambapo azote zina wapangaji na kuwa sehemu muhimu ya
kuongeza mapato ya shirika.
Aidha ameushauri uongozi wa AICC kuzingati uwekaji
wa miundombinu ya walemavu katika miradi mingine inayotekelezwa ukiwemo mradi
wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa kwa ajili ya maonesho ambao unatarajiwa
kukamilika mwezi Mei mwaka huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa AICC,
Elishilia Kaaya aliieleza Kamati ya PIC kuwa Kituo kina mipango ya baadae ya
kujenga Kituo kingine cha Kisasa cha Mikutano kitakachojulikana kama Mount
Kilimanjaro International Convention Centre (MKICC) ili kukabiliana na
ushindani wa biashara ya mikutano kutoka nchi za jirani kama Rwanda ambayo
tayari ina Kituo cha kisasa cha Kigali na Kenya ambayo tayari inatarajia
kujenga Kituo cha kisasa cha Mikutano huko Mombasa.
Kaaya ameeleza kuwa AICC imefanikiwa kununua ekari
23 katika mji wa Mtwara na pia inatafuta ardhi katika mikoa ya Dodoma, Mwanza
na Iringa kwa ajili ya kujenga Vituo vingine vya Mikutano. Aidha alieleza
Kamati kuwa mbali na kujenga Vituo vya Mikutano, AICC inatarajia kujenga
miundombinu kwa ajili ya Wanajuiya ya Kidiplomasia eneo la Laki Laki nje kidogo
ya mji wa Arusha ambapo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki imetenga eneo kubwa kwa ajili ya taasisi mbalimbali za kimataifa
kujenga ofisi.
Mbali na biashara ya mikutano, AICC
inajishughulisha pia na upangishaji wa ofisi na nyumba na pia inatoa huduma za
afya kupitia hospitali yake. Pia AICC inamiliki Kituo cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNICC) kilichopo Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment