Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amemtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki
Tundu Antiphas Lissu, ajitokeze ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na
tukio la kupigwa risasikwa bosi wake.
Mbunge Tundu Lissu.
|
Kamanda huyo amesema kwamba sababu
ya kumtafuta dereva huyo aliyemtaja kwa jina moja la Adam ni kwa sababu alikuwa
pamoja na majeruhi wakati tukio hilo linatokea lakini tangu kutokwea kwa tukio
hilo dereva huyo hajaonekana.
"Tangu kutokea kwa tukio dereva hakuonekana. Lakini kupitia gazeti
tumeona ameanza kufanya mahojiano jana. Sasa amewezaje kufika Dar es
salaam na Dodoma asifike. Sababu za kutoonekana hazifahamiki. Dereva huyo
ni mtu muhimu kwetu katika kutoa ushahidi. Natoa 'notice' afike ofisi ya
Mkurugenzi wa makosa ya jinai Dar au ofisi ya Mkuu wa makosa ya jinai Dodoma
atupe taarifa zinazohusiana na tukio hili. Tunaamini anazo siri za tukio hilo.
Kamanda Muroto ameongeza kuwa "Sheria yetu
inasema mtu aliye na taarifa akashindwa kuzitoa kwa jeshi la polisi atakuwa
amefanya mako. Na kwa nini asitoe.
Pia Kamanda huyo alimtaka Katibu
Mkuu wa Chadema Dkt. Vicent Mashinji kufika kwa RCO mjini Dar es Salaam ama
Dodoma kutokana kauli yake kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini wahusika.
Amemtaka kutoa taarifa kwa jeshi la
polisi kwa sababu kuonekana kwenye magazeti haitoshi bali kushirikiana kama
mwananchi ndiyo njia sahihi ya kuwabaini wahalifu.
Pamoja na hayo Kamanda Muroto
ameongeza kuwa "Tukio hili lisichukuliwe kama mtaji wa kisiasa. Nimesikia chama
fulani kinahamasisha watu kutoa damu. Nawaomba watulie watuachie polisi nafasi
ya kufanya kazi yetu. Matokeo mengi yameshatokea ikiwepo mauaji ya Kibiti,
Mauaji ya Askari wetu lakini jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na
kubaini".
G
0 comments:
Post a Comment