ASKOFU GWAJIMA NA WENZAKE WAFUTIWA MASHTAKA

Mahakama ya Mkazi Kisutu leo imemuachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa kufuta kesi yake ya kushindwa kutunza silaha baada ya mahakama kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo, na kuamuru arudishiwe mkoba wenye silaha yake.

Askofu Gwajima na wenzake watatu wamefutiwa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkehe.

Katika kesi hiyo ambayo Gwajima na wenzake watatu walikuwa wakisimamiwa na Wakili Msomi, Peter Kibatala, walishtakiwa kwa kosa la kumiliki Bastola aina ya Berretta yenye namba za siri CAT 5802 , Risasi 3 za pisto na risasi 17 za shortgun bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mamlaka husika mnamo Machi 29, 2015, katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A, jijini Dar es salaam.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment