Mwanafunzi Sophia Juma, wa St Marry Mazinde Juu ya Tanga ameibuka
kidedea katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa leo Jumamosi, Julai
15, akishika namba moja kitaifa.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa
(Necta), Dk Charles Msonde imeeleza kuwa nafasi ya pili imeshikwa pia na
msichana, Agatha Julius Ninga wa Tabora Girls. Wote walikuwa wakichukua masomo
ya mchepuo wa Sayansi (PCB).
Jumla ya watahiniwa 75,116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu huku wasichana
wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya
mtihani, waliofaulu ni 27,577 (sawa na asilimia 97.21). Kwa upande wa
watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34)
kati ya 46,385 waliofanya mtihani.
“Mchanganuo wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa
walipata daraja la 1-11 umepanda kwa
asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi 93.72 mwaka huu,” ilisema taarifa hiyo
Msonde aliongeza kwa kusema kuwa ufaulu wa wasichana umeongezeka
ikilinganishwa na wavulana,
“Pia ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda
ikilinganishwa na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07
ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.” ilisema taarifa hiyo
0 comments:
Post a Comment