Baraza la mitihani la Taifa (NECTA) imewafutia matokeo ya kidato cha
sita watahiniwa 10 baada ya kufanya udanganyifu katika mitihani yao.Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk
Charles Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao
kumi waliofutiwa matokeo, saba ni wa shule na watatu ni wa kujitegemea.
Pamoja na hao kumi, watahiniwa wengine 15 hawakufanya mitihani ya
baadhi ya masomo kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo
kushindwa kufanya mitihani hiyo.
‘Watahiniwa hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita,
Mei 2018 kama watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.
Pia, wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na
kushindwa kufanya mitihani yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei
2018.
0 comments:
Post a Comment