Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa
ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa
zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi.
Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa ulianza mwezi Machi 2017 na sasa tayari umekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani.
Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa ulianza mwezi Machi 2017 na sasa tayari umekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa akikata utepe kuzindua rasmi zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani
Lindi iliyojengwa
na Shirika la Nyumba (NHC)
|
Waziri
Mkuu alitoa pongezi hizo Alhamisi, Julai 13, 2017 alipozungumza na wananchi wa
kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo
iliyosimamiwa na NHC.
Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati wa
Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma
karibu kwa wananchi wake
“Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono".
“Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono".
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
NHC, Bw. Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa
na NHC na umegharimu sh. milioni 65.5.
“Shilingi milioni 15 zilitolewa na Rais. Dkt. Magufuli, sh. milioni 10 zilitolewa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye, NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri".

Awali Mbunge wa jimbo la Mtama,
Mheshimiwa Nape alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa
katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo.
Mheshimiwa Nape alisema
zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakati wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine
wanaoishi kwenye maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho.
0 comments:
Post a Comment