Waziri wa Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ametengua uteuzi wa wajumbe wote saba wa bodi ya NEMC na kumteua Dkt.
Elikana Kalumanga (UDSM) kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba |
Makamba amesema sababu za
utenguzi wa baraza hilo ni Ucheleweshwaji
wa kibali cha ukaguzi wa Mazingira, Tuhuma za rushwa katika usimamiz, Watendaji
wa NEMC kusaidia baadhi ya watu wenye maslahi nao.
Waziri Makamba amesema kuwa waliitaka NEMC waeleze jinsi wanavyofanya
kazi lakini hawakufanya hivyo.
Watendaji hao wamechukuliwa hatua baada ya uchunguzi wa kutosha huku hatua
nyinginezo zikifuata baadae.
“kutokana na mapungufu makubwa ndani ya NEMC, tumeamua kuvunja bodi
hii kuanzia leo na viongozi wengine tutawatangaza leo huku baadhi ya watendaji
wa NEMC tumewasimamisha kazi ili ufanywe uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili
kabla ya kuchukua hatua” amesema Makamba
Ameongeza kwa kusema kuwa kwa kuanzia sasa muwekezaji atakayekamilisha
kutoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda, ruhusa ya ujenzi itatoka ndani ya siku tatu
tu, na kwamba wawekezaji wanaokwenda NEMC watatkiwa kuaznia kwa washauri
elekezi ili kuondoa uhusiano wao na watu wa Baraza la NEMC.
0 comments:
Post a Comment