MAKADA WAKONGWE WAFUKUZWA CCM


Mapya yameibuka huko makau makuu ya nchi na chama tawala (CCM) kwenye kikao cha halmashauri kuu ya taifa kilichofanyika leo Machi 11 baada ya ya kikao hiko kuwachukulia hatua za kinidhamu makada wake ikiwemo kuwafukuza, nakuwaachisha uongozi baadhi ya makada wa chama hiko wakiwemo wenyeviti wa mikoa, wilaya, jumuiya na baadhi ya waumbe wa halmashauri kuu ya chama hiko.

Wanachama wenyeviti wa mikoa walofukuzwa ni Jesca Msambatavangu, mwenyekiti mkoa wa Iringa, ndugu Erasto Izengo Kwilasa, mwenyekti mkoa wa Shinyanga, ndugu Ramadhan Madabida, mwenyekiti mkoa wa Dar na ndugu Christopher Sanya, mwenyekiti mkoa wa Mara.

Pia miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye kikao hiko ni pamoja na taarifa ya masuala ya maadili ya Viongozi na kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya makada wake ikiwemo ya kuwafukuza, ambapo wajumbe wafuatao wa kamati kuu wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo Ndugu Emmanuel Nchimbi ambaye amepewa onyo kali na kutakiwa kuomba radhi, ndugu Adam Kimbisa amesamehewa makosa baada ya kuomba radhi, kujirekebisha na kuwaongoza vyema wanachama wa CCM Mkoa wa Dodoma kupata ushindi wa uchaguzi mkuu.

Wajumbe wa halmashauri kuu waliochukuliwa hatua za kinidhamu ni pamoja na ndugu Ali Hera Sumaye ambaye alikuwa mjumbe wa halmashauri Kuu kutoka Babati mjini amefukuzwa uanachama, Mathias Erasto Manga mjumbe wa halmashauri kuu taifa kutoka Arumeru kikao kimeamua afukuzwe uanachama, Ajiri Kalolo mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM kutoka Tunduru kikao kimeamua kumuachisha uongozi, na Valerian Alen Bureta mjumbe wa NEC kutoka Kibaha Vijijini ambapo kikao kimeamua kumuachisha uongozi


Wenyeviti wa wilaya ambao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ni pamoa na Omary Awadh mwenyekiti wa CCM wilaya ya Gairo kikao kimeamua kumfukuza uanachama , Ali S. Msuya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Babati Mjini kikao kimeamua kumfukuza uanachama, Makolo S. Laiza mwenyekiti wa CCM wilaya ya Longido kikao kimeamua kumfukuza uanacham, Abel Kiponza mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Mjini kikao kimeamua kumuachisha uongozi, Salumu Kondo Madenge mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni kikao kimeamua kumufukuza uanachama, Asa Simba Harun mwenyekiti wa wilaya ya Ilala kikao cha halmashauri kimeamua kumuachisha uongozi, Alfred S. Molel mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Mjini kikao kimeamua kumfukuza uanachana, Hamis J. Nguli mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Mjini kikao kimeamua kumuachisha uongozi, Muhaji Bushako mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muleba huyu amepewa onyo kali.

Katibu wa itikadi na uenezi Mhe. Humphrey Polepole amesisistiza ya kwamba kikao cha kamati kuu pia kilitazama jumuiya zake wapo viongozi pia wamepatikana na hatia ya maadili ikiwemo Mhe, Sophia Simba ambaye ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania pia amechukuliwa hatua kwa kufukuzwa uanachama baada ya kukutwa na makosa ya kinidhamu, huku Josephine Genzabuke mbunge na mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kigoma akipewa onyo kali.


Katika kikao hiko pia halmashauri Kuu ya Taifa imeunda Kamati chini ya makamu mwenyekiti Mzee P. Mangula kufanya tathmini ya kina juu ya hali ya kisiasa Zanzibar. Katibu wa itikadi na uenezi alimaliza kwa kusema "Adhabu hizi zilizotolewa na Kamati Kuu hazina rufaa, ndio tumefika mwisho na zinaanza kutekelezwa leo"

Chama cha mapinduzi chini ya mwenyekiti wake mpya Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Katinu muenezi Humphrey Polepole wamedhamiria kufanya mapinduzi ndani ya chama hicho kupitia kauli zao ambazo mara kadhaa wamesikika wakizungumza.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment