Maafisa wanasema kuwa vifaa
hivyo ambavyo ni vikubwa ikilinganishwa na simu aina ya Smartphone
havitaruhusiwa katika ndege ya abiria kwa kuwa huenda vinaweza kubeba vilipuzi.
Ni kampuni moja ya ndege pekee
inayoruhusu vifaa hivyo kutumika hadi mtu anapoabiri ndege.
Marufuku hiyo inasimamia mataifa manane huku Uingereza ikitoa
marufuku kama hiyo vifaa hivyo kutoka kwa mataifa sita.
Kampuni tisa kutoka mataifa
manane -Uturuki, Morocco, Jordan, Misri, UAE, Qatar, Saudia na Kuwait
zimeathiriwa na marufuku hiyo ya Marekani.
Mataifa hayo huendesha safari
50 za ndege kuelekea Marekani.
Ndege za miliki ya kiarabu UAE
hutoa huduma ya kusafirisha mizigo kupitia ndege na meli katika milango ya
viwanja vya ndege ili kuwawezesha abiria kutumia vifaa vyao vya kielektroniki
baada ya kuiingia katika eneo la kusubiri ndege hadi wanapoingia ndege.
Hiyo inamaanisha kwamba abiria
wanaosafiri mara mbili kutoka mataifa mengine kuelekea Marekani kupitia Dubai
wanaweza kutumia vifaa hivyo vya kielektroniki katika safari ya kwanza.
Marufuku ya Uingereza inaathiri
ndege zote kutoka Misri, Uturuki, Jordan, Saudia, Tunisia na Lebanon.
0 comments:
Post a Comment