Miili hiyo ilipatikana eneo
ambapo raia wa Marekani Michael Sharp na raia wa Sweden Zaida Catalan walitekwa
nyara wiki mbili zilizopita. Miili hiyo ni ya mwanamume na mwanamke ambao wote
ni wazungu.
Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa walikuwa nchini DRC kufuatilia
vikwazo vilivyowekwa dhidi DRC, lakini wakati huo walikuwa wakichunguza ripoti
za dhuluma eneo la Kasai.
Msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende, alithibitisha ripoti
za kupatikana kwa miili hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa
uchunguzi wa DNA unahitaji kuondoa shaka yoyote kuhusu miili hiyo.
Serikali ya Congo inapigana na kundi la waasi ambalo linahudumu
eneo hilo na linaaminiwa kuwateka wataalamu hao.
Ghasia eneo la Kasai
zimechochewa kufuatia kuuliwa kwa kiongozi wa kitamaduni Kamuina Nsapu, ambaye
alikuwa akiongoza upinzani dhidi ya Rais Joseph Kabila
0 comments:
Post a Comment