Mwanamke huyo hakupigwa risasi,
kwa mujihu wa msemaji wa polisi mjini Washington.
Alikamatwa na kisa hicho
kikasababisha kufungwa kwa moja ya majengo ya bunge.
Kisa hicho kinajiri baada ya kushuhudiwa mashambulizi kadha ya
kugonga kwa magari miji ya London na Brussels,
Msemaji wa polisi Eva Malecki,
amesema kuwa mshukiwa ni mwanamke na kisa hicho ni cha uhalifu.
Kisa hicho kilitokea wakati maafisa waligundua dereva ambaye
alikuwa akiendesha gari kwa njia isiyo ya kawaida na kutaka kumsimamisha.
Dereva huyo kisha akageuza gari kwa haraka na nusura awagonge
polisi.
Sababaua ya kisa hicho haijulikani na mwanamke huyo
hajatambuliwa.
Vikao vya bunge vinaendelea kama kawaida na watalii wameruhusiwa
kurudi eneo hilo.
0 comments:
Post a Comment