Mkurugenzi wa vipindi na
vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group leo amethibitisha kwamba RC Makonda
alivamia katika ofisi za Clouds Media Group. Alizungum. Alizungumza hay oleo
asubuhi katika kipindi cha Clouds360 mbali na hayo mkurugenzi huyo ameonesha
kusikitishwa na tukio hilo na kwamba hakutegemea kama RC Makonda angefanya
hivyo .
“Mtangazaji mmoja
alinifuata akaniambia wamefanya mahojiano na mwanamke anayedaiwa kuwa amezaa na
Askofu Gwajima lakini Gwajima mwenyewe hawajampata. Niliwaambia watangazaji
kama hawajampata Gwajima basi kipindi hicho kisirushwe kwa kuwa hakina
‘balance’ na wamwambie Makonda”
“Gwajima alinipigia simu
akisema amesikia kuwa kuna kipindi chake, nikamwambia kuwa hakitarushwa kwa
sababu hatujasikia pande zote. Na nikampigia simu mkuu wa vipindi kumwambia
ahakikishe kuwa kipindi hicho hakirushwi kwa vile hakijabalance”
“Ijumaa saa 5 usiku
nikapigiwa simu na Afisa Rasilimali watu wa Clouds kuwa Makonda amekuja ofisini
akiwa na askari na wana bunduki, mlinzi hakusita kumruhusu aingie kwa vile
amemzoea Makonda, ila alishtushwa na askari wale waliokuwa na bunduki”
“Nilimwambia mlinzi
aende kule juu studio aone kuna nini na alipokwenda alimkuta Makonda anachukua
kipindi kwenye ‘flash’ kasha akaondoka nayo, hakuna kijana yeyote aliyepigwa
usiku ule lakini tatizo kubwa ni namna tukio lilivyotokea”
Akizungumzia kuhusus
CCTV kamera, alisema ni kweli wana CCTV ofisini kwao kwa sababu ni chombo cha
habari, japo hajui ni nani aliyerusha na kusambaza video inayomuonesha Makonda
akiingia Clouds akiwa na askari wenye bunduki.
“Ni
kweli pale Clouds na sijui kaachia nani zile video, Ni kweli tuna Cctv kila
sehemu maana hili ni jengo la habari“
Lakini pia aliongeza kwa
kusema kuwa wamekuwa na uhusiano mzuri na Makonda na serikali na hawataki
uhusiano huo ufe bali kuendelea kuzitangaza ajenda za kimaendeleo zitakazoletwa
na seriali.
“Sijutii
ukaribu wangu na Paul Makonda lakini nakwazika na kuvunjiana heshima. Kitu kibaya ambacho kinaumiza moyo Makonda
ametumia vibaya madaraka yake pamoja na urafiki wake kwetu. Makonda ni mdogo
wangu sana anaweza kuniomba msamaha, akumbuke mm nawakilisha kundi la watu
waliokosewa kwenye hili”
“Hatua
ya maamuzi yetu bado tupo kwenye mashauriano hatutaki kupingana na ajenda za
serikali kwa sasa, tutaamua cha kufanya. Sisi sio viongoz ni Wananch tuna zaid ya miaka 19 kama chombo
cha Habari tunakaribisha Agenda zenye ubunifu njooni tujadiliane pamoja”.
0 comments:
Post a Comment