Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu watano akiwemo
mfanyabiashara Gerald Kimario ambaye anashikiliwa kwa kosa la kufanya
biashara ya pombe aina ya viroba na kukutwa na vifungashio vya pombe hiyo.
Watuhumiwa wane wamekamtwa kwa kosa la usafirishaji wa dawa za kulevya na unang’anyi.
Jeshi hilo mbali na kuwakamata watuhumiwa hao, limekata silaha, dawa za kulevya, pombe aina ya viroba ambayo imepigwa marufuku kuuzwa pamoja na vifungashio vyake, na gari aina ya Scania ambayo ilikuwa ikisafirishia dawa za kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi ,Wilbroad Mutfungwa akionyesha silaha
zilizomakamatwa pamoja na Dawa za Kulevya aina ya Mirungi na Bhangi.
|
Mkaguzi wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa,William Mhifadhi akitizama Pombe iliyopigwa marufuku ikiwa
katika vifungshio vya plastiki
|
Dawa za kulevya aina ya Mirungi iliyokamatwa.
|
Sehemu ya Vifungashio vya Plastiki vya Pombe
viivyoppigwa marufuku hivi karibuni.
|
Silaha aina ya Bastola zilizokamatwa na jeshi
hilo
|
Misokoto ya Bhangi iliyokamatwa.
|
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia
taarifa ya Kamanda wa Polisi,(hayupo pichani.)
|
Watuhumiwa wa matukio ya usafirishaji wa Dawa
za kulevya pamoja na Unyang'anyi wakiwa mikononi mwa jeshi la Polisi.
|
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad
Mutfungwa akionesha gari lililokamatwa likiwa na mizigo ya Dawa za kulevya aina
ya Milungi ,wahusika wakijaribu kuisafirisha.
|
0 comments:
Post a Comment