Naibu waziri wa mambo ya nje
wa Korea Kaskazini Sin Hong Chol amesema wataendele kufanya majaribio ya
kurusha makombora kila siku huku akiitishia Marekani kwa kusema kama wanapanga
mashambulizi ya kijeshi wao watajibu kwa nyuklia katika mtindo wanaoujuwa wao.
Wazii huyo amezungumza hayo
alipokuwa akihojiwa na mwanahabari wa BBC John Sudworth
“Tutaendelea kufanya
majaribio ya makombora, kila siku, mwezi na kila mwaka” akaongeza kwa kusema “kama
Marekani inapanga shambulizi la kijeshi dhidi yetu, sisi tutajibu kwa nyuklia
katika mtindo tuujuao sisi wenyewe” Alisema Sin
Kumekuwa na majibizano kati
ya Korea Kaskazini kwa siku kadha tangu Marekani ipeleke Meli za kijeshi katika
rasi ya Korea, hali hii imepelekea hali ya wasi wasi kati ya nchi hizo mbili na
hata ulimwengu juu ya uwezekano wa kutokea vita kubwa.
0 comments:
Post a Comment