Mvua
zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo nchini zimesababisha maafa
katika maeneo kadha ikiwemo katika wilaya ya Chalinze ambako makazi ya watu
yameharibiwa kutokana na mvua hizo, eneo la Chalinze mzee, Bwawa la umwagiliaji
la Msoga na Shule ya Sekondari ya Imperial yameathirika na mvua hizo.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amelazimika kwenda jimboni kwake
kushuhudia maafa hayo, pia ametoa pole kwa wakazi hao na kuwataka wawe
wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Mbunge
huyo ameeleza kwamba madhara makubwa yaliyosababishwa na mafuriko hayo ni
kuharibika kwa mashamba, nyumba za wananchi na kusababisha wakazi wa maeneo
hayo kwa takibani kaya kukosa mahala pa kulala.
Mbunge
wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete (aliyevaa kanzu) akitazama athari za mvua
ambazo zimesababisha bwawa la umwagiliaji la Msoga kuharibika
|
Baadhi
ya nyumba ambazo zimeathirika na maafa ya mvua Chalinze Mzee
|
Sehemu
ya bwawa la umwagiliaji la Msoga ambalo limeharibiwa kutokana na mvua
zinazoendelea jimboni humo
|
Nyumba
iliyopo Chalinze Mzee ambayo imeharibiwa na mvua
|
Nyumba
iliyopo Chalinze Mzee ambayo imeharibiwa na mvua
|
Baadhi ya nyumba ambazo zimeathirika na maafa ya mvua Chalinze Mzee
|
Mbunge
Ridhiwani Kikwete akijaza kitabu cha mahudhurio pindi alipofika katika kijiji
cha CHalinze Mzee
|
0 comments:
Post a Comment