ROMA ASIMULIA TUKIO LA KUTEKWA KWAKE

Msanii wa muziki wa hip hop hapa Tanzania maarufu kwa jina la Roma Mkatotili leo ameeleza kwa kina jinsi tukio la kutekwa kwake na wenzake lilivyotokea mpaka kufikia kupatikana katika kituo cha polisi Ostabei. Msanii huyo alitekwa siku ya Jumatano majira ya saa moja usiku yeye na wenzake katika studio ya Tongwe ambapo ndiko anakofanyia kazi zake za muziki.

Msanii Roma alieleza tukio hilo leo mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa habari maelezo, Roma ameeleza kwamba siku ya tukio waliwajia watu studio wakiwa na silaha za moto, waliwafunga pingu, vitambaa vyeusi usoni na kuwaingiza kwenye gari na kuwapekelekwa sehemu isiyofahamika ambapo walifanyiwa mahojiano, na baada ya kumaliza mahojiano  walifungwa midomo, miguu na mikono na baadae kutupwa sehemu isiyojulikana.


Roma aliendelea kusimulia kwa kusema, kwa kuwa wailkuwa wamefungwa iliwachukua muda kujifungua, lakini walifanikiwa kujifungua na kuanza kutembea bila ya kujua wapi walipo na hatimaye walifanikiwa kukiona kibao kilichoandikwa ‘UNUNIO’ ndicho kilichowasaidia kutambua kwamba wapo Dar, Roma na wenzake walichukua pikipiki na kuelekea nyumbani kwake (Roma), lakini kwa sbabu za kiusalama waliamua kwenda kuripoti kituo cha polisi, Alisimulia Roma Mkatoliki

Hata hivyo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harryson Mwakyembe ameonesha kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kulifuatilia suala hiyo kwa ukarib. Pia waziri huyo amezungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto ambazo wasanii wanakutana nazo na kusema kwamba yeye kama waziri anawathamini sana wasanii na anathamini kazi wanayoifanya kuiwakilisha Tanzania.
“Mimi nawathamini sana hawa wasanii, wanapeperusha bendera ya Tanzania” alisema waziri Mwakyembe


Pia aliongeza kwa kusema kilichotokea hakivumiliki maana si kitendo cha kawaida huku akisisitiza kulifuatilia jambo hilo kwa haraka.
"Hiki kilichotokea siyo hali ya kawaida kwa watanzania, hatuwezi kukubali kitu kama hiki kiendelee kutokea,nitalifuatilia kwa ukaribu sana, nitajitahidi nipate majibu kabla ya bajeti yangu Bungeni". Alisema Dk. Mwakyembe

Pia waziri huyo amewaomba wananchi kutoamini maneno ambayo yanazungumzwa na watu bila ya kuwa na uhakika wa mambo hayo, na amewataka waandishi na vyombo vya habari kuwahoji wasanii bila ya kuwa na taarifa kamili kutoka kwake.

Naye msanii Roma mbali na kuelezea tukio hilo kwa ufupi amesema mambo mengine hatoweza kuyazungumza kwa sasa kwa suala hilo lipo mikononi mwa polisi na linafanyiwa kazi ili kupata taarifa kamili ya tukio hilo

"Kwa kuwa tumeshatoa maelezo yote polisi, leo sitaongea sana maana nikisema mengine itakuwa ni kuingilia upelelezi" Alisem Roma Mkatoliki
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment