Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imeadhimimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanizibar ambao
uliunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukio hilo la mmuungano lilifanyika
mnamo mwaka 1964 April 26 ambapo lilijumuisha uchanganyaji wa udongo kutoka
Tanganyia na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru Dar es salaam.
Kama ilivyo miaka yote
sherehe za muungano hufanyika huku zikipambwa na burudani kutoka vikundi mbali
mbali vya sanaa, maonesho ya halaiki pamoja na maonesho ya makomandoo ya
kuonesha ukakamavu na namna ya kumkabili adui, ambapo sherehe hizo kwa mwaka
huu zimefanyika makao makuu ya cnhi mjini Dodoma ambako serikali iko kwenye
mchakato wa kuhamia huko.
Katika maadhimisho hayo ya
miaka 53 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais
wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alihutubia
mamia ya wananchi wa mkoa wa Dodoma waliohudhuria katika maadhimisho hayo mjini Dodoma.
Katika hotuba yake Rais
Magufuli amewaonya wale wanaojaribu kutaka kuvuja muungano ya kwamba
watavunjika wao "Nataka niwahakikishie mimi na Dr. Shein tutaulinda
Muungano kwa nguvu zote, atakayejaribu kutaka kuuvunja atavunjika yeye" alisema Rais Magufuli
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya
pili Mzee. Ally Hassan Mwinyi
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli akisalimiana na mke wa muasisi wa Muungano Mwl. Julius Nyerere
|
0 comments:
Post a Comment