WATU MILIONI MOJA SUDANI KUSINI HATARINI KWA BAA LA NJAA

Baa la njaa mchini Sudan ya Kusini huenda likazidi kutokana na kuongezeka kuwapo na mahitaji ya chakula huku upatikanaji wa chakula ukiwa finyu. Watu laki moja nchini humo wanakabiliwa na ukosefu wa chakula huku miongoni mwa sababu zinazotajwa ni mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea.

Mtoto anayekabiliwa na utapia mlo kutokana na ukosefu wa chakula
Taarifa hizo zimetolewa na Umoja wa Mataifa kupitia mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini Bw. David Shearer, pia ameonya kuwa endapo jitihada za makusudi na haraka hazitachukuliwa njaa inaweza kuenea zaidi katika maeneo mengi nchini humo.

Mmoja wa wahanga wa baa hilo la njaa nchini humo, ambaye pia ni mama wa watoto watatu, Maria Nyamuoka amesema muda mwingine hulalamika kwamba wanahisi njaa lakini hukosa cha kuwapa watoto hao,
“watoto hulalamika kila mara kamba wanahisi njaa, lakini sina cha kuwapa” alisema Maria
Taarifa kutoka Umoja wa Mataifa zinasema watu Milioni moja wapo kwenye hatari ya kukumbwa na baa hilo la njaa mbali na watu laki moja ambao tayari wamekumbwa ukosefu wa chakula, pia imeelezwa kwamba watoto alio chini ya umwi wa miaka mitano wako kwenye hatari kubwa zaidi ya kuathirika na ukosefu wa chakula kutokana na kuwa na kinga dhaifu. Pia zaidi ya watu Milioni 5 wanategemea chakula cha msaada nchini humo.


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment