ARSENAL YAPANDA DARAJA BAADA YA KUITANDIKA SOUTHAMPTON MBILI BILA

Timu ya Arsenal imepanda daraja baada ya kuichapa bao mbili kwa bila timu ya Southampton, magoli ambayo yalitiwa wavuni na wachezaji Alexis Sanches ambaye aliipatia Arsenal goli la kwanza mnamo dakika ya 60 huku Olivier Giroud akiwaongezea machungu Southampton baada ya kuongeza bao la pili mnamo dakika ya 83.
Kutokana na ushindi walioupata Arsenal katika mechi yao ya jana wamepanda daraja mpaka nafasi ya tano na kuwa juu kwa daraja moja zaidi ya timu ya Manchester United wakiwa na jumla ya pointi 69 huku Manchsetser United wakiwa na jumla ya point 66.
Bossi wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema walikuwa wamejipanga vizuri na walilenga kwenye ushindi huku wachezaji wote wakicheza mchezo wenye shauku ya kutaka ushindi.
“Tulikuwa tuna malengo na nilihisi hilo kwani tunapokuwa na hali ngumu huwa tunakuwa pamoja” “tuna ukurasa upya na ninajua tunaweza kusonga mbele na kushinda magoli zaidi, timu yote ilikuwa iko tayari kwenda na mabadiliko, ilikuwa na malengo na kuonesha shauku ya kutka kuchinda mchezo” amesema Wenger
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment