Simba Sports Club imeibuka
Bingwa wa kombe la Azam Sposts Federation Cup (ASFC) baada ya kuichapa timu ya
Mbao FC bao 2 kwa bila katika mchezo wa fainali uliochezwa kati ya Simba SC na
Mbao FC katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Mechi hiyo iliyoonekana ngumu
kati ya mahasimu hao wawili katika dakika tisini za kisheria za mchezo huo, na
kumlazimu refa aliyekuwa akichezesha mchezo huo kuongeza nusu saa ya ziada
ndipo ambapo ilipelekea kuwepo kwa unafuu wa mchezo huo kati ya timu zote mbili
ambapo timu ya Simba SC ilijipatia magoli yake katika dakika hizo za nyongeza
huku Mbao FC ikijipatia goli la kufutia machozi katika dakika hizo za nyongeza.
Mnamo dakika ya 95 ya mchezo
huo timu ya Simba ilijipatia goli lake la kwanza kupitia mchezaji wake
machachari kabisa wa kimataifa Blagnon huku goli la pili likifungwa na Shiza Ramadhani Kichuya kwa mkwaju wa penati
mnamo dakika ya 120. Nao Mbao FC walipata goli lao la kufutia machozi ambalo lilitiwa
wavuni na mchezaji Ndaki Robert.
Klabu ya Simba inakuwa timu
ya pili kutwaa kombe la Azama Federation tangu kuanzishwa kwake dada ya Yanga
FC kuchukua kombe hilo katika msimu wa kwanza. Kufuatia ushindi wa leo Club
ya Simba wanapata na kitita cha Tsh. Mil. 50 na nafasi ya kuiwakilisha Tanzania
katika Kombe la Shirikisho barani Afrika
0 comments:
Post a Comment