Klabu ya soka ya Dar es
salaam Young African (YANGA) imethibitisha deni ambalo inadaiwa na wizara ya
ardhi Shilingi Milioni 300 ikiwa ni kodi ya jengo la ofisi za kilabu hiyo.
Katibu mkuu wa Kilabu hiyo Charles
Boniface Mkwasa amethibitisha suala hilo kuwa tangu mwaka 1997 kilabu hiyo
haikuwah kulipa kodi ya ardhi na kusema kwamba wanafanya kila jitihada
kuhakikisha wanalipa deni hilo
“Ni muda mrefu kodi hii
ilikuwa haijalipwa, kipindi hicho kodi ilikuwa ni rahisi ;lakini miaka ya
karibuni imekuwa ikiongezeka na kama ninavyosema na tunatakiwa kulipa Milioni
56 na laki 6 kwa mwaka. Sisi kama uongozi tunafanya jitihada kubwa za kuweza kulinusuru
jingo letu na Mungu akijalia itawezekana ” alisema Mkwasa
0 comments:
Post a Comment