Korea Kusini imesema ndege mbili za kivita za Marekani
zenye uwezo wa kutupa mabomu ardhini zimeruka katika anga la rasi ya Korea.
Ndege hizo mbili aina ya B1-B zimeshiriki pamoja na ndege za kivita za Korea
Kusini.
Rais wa Marekani Donald Trump alisema kuwa yuko tayari kufanya
mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un iwa mazingira yataruhusu
kufanya hivyo, naye msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema kwamba Mazingira kama
hayo unaweza kutowakutanisha Trump na Kim.
Rais Donald Trump amesema kuwa Korea Kaskazini inafanya vitendo
vya kukera kutokana na mpango wake wa kutaka kuendelea kufanya majaribio ya
makombora ya nyuklia.
Nayo Korea Kaskazini imeendelea kuongeza kasi yay a kufanya
majaribio ya Makombora yake na silaha nyingine za nyuklia japo Umoja wa Mataifa
tayari umepiga marufuku nchi hiyo kuendelea kufanya majaribio hayo.
Pia Korea Kaskazini inaamini kwamba silaha zake za
nyuklia zinaweza kuilinda nchi hiyo dhidi ya shambulio la kijeshi kutoka kwa
nchi ya Marekani na kile kinachoaminika kuwa Marekani na Korea Kusini
zinaweza kuunganisha na kumuondoa
madarakani Rais wa nchi hiyo Kim Jong-Un
0 comments:
Post a Comment