Rais Magufuli ameongoza sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi
Duniani Mei Mosi, maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Chuo Cha
Ushirika Moshi MoCU na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mama Samia Sluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala
Bora, Angela Kairuki, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
Jenista Joakim Mhagama, Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tumaini
Nyamhokwa na shirika la kazi Duniani ILO.
Maandamano ya wafanyakazi yamejumuisha wafanyakazi kutoka ofisi, mashirika na
idara mbalimbali za serikali yakiongozwa na wafanyakazi kutoka ofisi ya Mkoa wa
Kilimanjaro
Katika hotuba ya Mgeni rasmi
katika maadhimisho hayo Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli imezungumzia mambo
kadha ikiwemo kumalizika kwa zoezi la uhakiki wa vyeti kwa 98% ambako
kutapelekea kuwepo kwa ajira za kutosha kufikia 52,000 na kuongezeka kwa
mishahara ya watumishi wa umma.
Pia Rais Magufuli
amesisitiza kuwa atatoa ushirikiano kwa vyama vya wafanyakazi na kusema kwamba wafanyakazi
kujiunga na vyama hivyo ni hiari nan i jambo la kisheria. Pia amewataka waajiri
wote kuhakikisha kuwa wanwaptia wafanyakazi mikataba kwani hilo I jambo la
kisheria na mwajiri asipofanya hivyo anakwenda kinyume na sheria.
Mbali na hayo Rais Magufuli
ametangaza kuanzishwa kwa bima ya ajira ambayo muswada wake utakapokamilika
utawasilishwa bungeni kujadiliwa ili u[itishwe. Amegusia suala la malimbikizo
ya michango ya michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo waajiri wamekuwa
wakilimbikiza bila kuwasilisha kwenye mifuko hiyo, kuwa ni jukumu la kila
mwajiri kuwasilisha michango hiyo kwa wakati, amesema kabla ya kuwawajibisha
waajiri wengine, ameanza na serikali na tayari kiasi kikubwa cha deni la
michango ya mifuko ya jamii limepunguzwa kwa kiwango kikubwa na ameahidi
kulimaliza.
Maandamano ya wafanyakazi wakipita mbele ya Rais
John Magufuli katika Viwanja vya ushirika mjini Moshi katika maadhimisho ya
siku ya wafanyakazi Duniani.
|
0 comments:
Post a Comment