Rais wa Sudan Kusini Salva
Kiir amemfuta kazi mkuu w a majeshi wa nchi hiyo Jenerali Paul Malong, mpaka
sasa hakuna sababu yeyote iliyotajwa kuachishwa kwake japo katika siku za
karibuni maafisa kadhaa wa juu katika jeshi na serikali ya Sudan Kusini
wamekuwa wakijiuzulu.
Jeneali Malong amekuwa
akishutumiwa kwa vita vya kikabila dhidi ya watu wa makabila ambayo hayana
nguvu nchini humo.
Rais Kiir alitangaza
kumfukuza kazi mkuu huyo wa majeshi katika Televisheni ya Taifa ambapo amemteua
aliyekuwa msaidizi mkuu wa utawala na fedha katika jeshi la Sudani Kusini kushika nafasi hiyo ya ukuu wa majeshi ya
nchini humo
Wananchi wa Sudan wanaamini
kuwa mkuu wa majeshi Jenerali Malong ana nguvu na uwezo wa kiushawishi hivyo
wanasubiri kwa hamu ni kwa namna gani aataitikia kuondolewa kwake katika nafasi
hiyo na Rais Kiir.
Kumekuwa na upendeleo na
mapigano ya vita vya kikabila nchini Sudani Kusini, huku makabila yenye nguvu
yakiwatenga na kuwanyima nafasi watu wanaotoka katika makabila yasiyo na nguvu
kisiasa na kiuchumi
0 comments:
Post a Comment