Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ameridhia maombi ya kuacha kazi kwa viongozi, Ndugu Saidi Meck Sadiki
ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Aloysius Kibuuka Mujulizi
ambaye alikuwa jaji wa mahakama kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania na Ndugu Upendo Hillary Msuya ambaye naye alikuwa
jaji wa mahakama kuu Tanzania.
Taarifa hiyo ya Rais kukubali maombi hayo imetolewa leo Jumatano
Mei 16 na Katibu mkuu kiongozi Balozi John Kijazi ambapo ridhaa hiyo ya rais
kukubali maombi ya viongozi hao kuacha kazi kuanzia tarehe 15 Mei 2017.
Ndugu Saidi Meck Sadiki ambaye alikuwa mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro
Ndugu Aloysius Kibuuka Mujulizi ambaye alikuwa jaji wa
mahakama kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania
|
Ndugu Upendo Hillary Msuya ambaye naye alikuwa jaji wa
mahakama kuu Tanzania.
|
0 comments:
Post a Comment