Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imetoa vibali vya kuajiri watumishi 15,000 katika kada
mbalimbali mwezi huu kufuatia zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi ambalo
limeleta upungufu wa watumishi serikalini na kupelekea baadhi ya huduma
kudhoofu katika upatikanaji wake.
Zoezi hilo lililofikia
tamati yake April 28 kwa awamu ya kwanza lilibaini jumla ya watumishi 9,932
wenye vyeti vya kughushi, watumishi 1,538 wenye vyeti vyenye utata kwa kuwa na
watumaji zaidi ya mmoja, huku watumishi 11,596 wakiwa na vyeti ambavyo
havijakamilika.
Watumishi 11,596 wenye vyeti pungufu wametakiwa kukamilisha
zoezi la kuwasilisha vyeti hivyo kabla ya Tar 15 Mei mwaka huu na watumishi 1,538
wenye vyeti vyenye utata nao wametakiwa
kuwasilisha ushahidi wa umiliki halali wa vyeti hivyo Baraza la Mitihani la
Taifa (NECTA) kabla ya tarehe 15 Mei.
Nalo zoezi la uhakiki wa
watumishi wa wizara ikiwa ni awamu ya pili ya uhakiki linatarajiwa kukamilika
kabla ya Tarehe 10 Mei 2017
0 comments:
Post a Comment