WAHUDUMU WA MONCHWARI WAIBA KETE 32 ZA DAWA ZA KULEVYA



Wahudumu wa monchwari katika Hospiali ya Mwananyamala wamedaiwa kuiba kete 32 za dawa za kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa marehemu uliofikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amethibitisha kuokea kwa tukio hilo na kusema kwamba raia huyo ambaye ana uraia wa nchi ya Ghana alifariki dunia akiwa kaika nyumba ya wageni ifahamikayo kwa jina la RED CARPET iliopo Sinza jijini Dar es salaam akiwa na kete hizo tumboni. 

Kamanda Sirro amesema wahudumu hao walioiba kete hizo 32 tayari wanashikiliwa na polisi pamoja na wanunuzi wa kete hizo amba alitajwa na wahudumu hao ambao waliwauzia kete hizo.
 "Yule Mghana ambaye alikutwa amefariki dunia tarehe 14/ 03/ 2017 kwenye nyumba ya wageni ya 'Red Carpet' na alichukuliwa na kupelekwa mochwari Mwananyamala lakini inaonekana wale wahudumu wali[pata taarifa kuwa ule mwili una dawa za kulevya, kimsingi walikula njama wakampasua na kutoa kete 32 za madawa ya kulevya na baada ya kuyapata waliyauza hayo madawa" amesema Kamanda Sirro
Kamnada Sirro aliongeza kwa kusema kwamba wanawashikilia watu wanne ambao walihusika kuupasua mwili wa arehemu na kutoa kete hizo 32, lakini pia amemtaja mnunuzi aanayejuikana kwa jina la Ally Nyundo ambaye aliuziwa dawa hizo za kulevya kutoka kwa mtu aliyezinunua kutoka kwa wahudumu wa Monchwari.
"Mpaka sasa tunawashikilia watu wanne ambao wanakiri kupasua mwili huo ambao ni wahusika wakuu na ni wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala lakini tumekwenda mbali zaidi baada ya kufanya upasuaji wamemuuzia nani naye amekamatwa pia na anaeleza kuwa alinunua hayo madawa, lakini pia naye alichukua na kumuuzia mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Ally Nyundo, huyu Nyundo tulishamkataga na kumpeleka kwa Mkemia Mkuu yeye alionekana ni mtumiaji, kimsingi tuna hao watuhumiwa wanne na huyo wa tano aliyekamatwa sasa tunaandaa jalada" alisisitiza Kamanda Sirro
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment