Serikali kupitia wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na
Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira imetoa ofa kwa watanzania wote
kutembelea hifadhi za mbuga za wanyama bila kulipa kiingilio kuanzia tarehe 2
hadi 4 ya mwezi Juni kufuatia maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani
inayoadhimishwa Tarehe 5 Mwezi June Duniani kote. Ambapo kwa mwaka huu 2017 kauli mbiu ya siku ya Mazingira
ni “Connecting
people to nature”
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) inawakaribisha
wananchi wote kuitumia ofa hiyo ambayo itajumuisha msamaha wa kiingilio na
ada ya magari, ambapo katika hifadhi ya Kilimanjaro ofa itakuwa ni ya siku moja
huku gharama za malazi, usafiri na huduma nyingine zinazotolewa na sekta
binafsi zikiwa hazipo kwenye ofa hiyo.
0 comments:
Post a Comment