Kampuni ya Barick Gold
Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acasia Mining Limited imekubali
kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kufanya malipo ya fedha
ambazo kampuni hiyo inadaiwa na serikali ya Tanzania baada ya kufanya kazi bila
kulipa kodi tangu kampuni hiyo ya Acasia ilipoanza kazi zake.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya
mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa kampuni ya Barick Gold Corporation Prof. John
L. Thornton na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Ikulu jijini Dar es salaam. Mazungumzo hayo yameshuhudiwa na Balozi wa Canada
nchini Tanzania Mhe. Ian Myles pamoja na waziri wa Katiba na Sheia Mhe.
Palamagamba Kabudi.
Prof. John L. Thornton amesema
kampuni yake iko tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi
ya pande zote mbili na kulipa fedha ambazo Tanzania ilipaswa kulipwa tangu
kampuni ya Acasia ilipoanza kufanya kazi Tanzania.
Rais Magufuli naye amekubali
kufanya mazungumzo na kampuni hiyo na kusema kwamba ataunda jopo la waaalamu
watakaojadiliana na kampuni hiyo kufikia makubaliano ya kulipwa kwa fedha hizo.
Pamoja na hayo Rais Magufuli
amevionya vyombo vya habari vinavyowataja marais wastaafu juu ya kuhusika
kwenye sakata la mchanga wa madini na kusema kuwa katika ripoti zote mbili hakuna
mahala kaika ripoti hizo palipowataja marais wastaafu.
“Nimesoma ripoti zote mbili
hakuna mahali ambapo Mze Mkapa na Mzee Kikwete wameajwa, vyombo vya habari
waache kuwachafua hawa wazee, wamefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa letu,
tuwaache wapumzike” Alisema Rais Magufuli
Mazungumzo hayo ni matokeo ya
kazi iliyofanywa na wataalamu wa Madini na Miamba ambao waliwasilisha ripoti ya
kiasi na thamani ya mchanga wa madini unaosafirishwa kwenda nje kwa ajili ya
uchenjuaji pamoja na ripoti ya pili ambayo ilifanywa na wataalamu wa sheria na
uchumi ambao waligundua mambo kadhaa ikiwemo upotevu wa fedha nyingi na mapato
ya serikali pamoja na kuwepo kwa mikataba mibovu na sharia dhaifu za madini na
shughuli za uchimbaji madini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment