Timu ya soka ya Real Madrid ya Hispania itacheza mchezo wa UEFA Super
Cup na timu ya Soka ya Manchester United kutoka Uingereza baada ya kuunyakua kombe
la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa goli 4 kwa 1 katika mechi iliyochezwa katika
uwanja wa Cardif kati yao dhidi ya Juventus jana.
Kufuatia ushindi huo kilabu ya Real Madrid ya Uhispania inaweka rekodi
ya kuwa kilabu ya kwanza kuchukua ubingwa huo mara mbili mfululizo.
Mabao ya timu ya Real Madrid yaliwekwa wavuni na Christian Ronaldo
ambaye alifunga mabao mawili bao la kwanza likiwa mnamo dakika ya 20 na bao lake
la pili katika dakika ya 64, mabao mengine mawili yalifungwa na Casemiro mnamo
dakika ya 61 huku bao la mwisho likifungwa mnamo dakika ya 90 na mchezaji
Asensio.
Goli la Juvenus lilifunga na Mandzukic mnamo dakika ya 27. Mechi hiyo iliyochezewa Cardiff ilikuwa ya 19
kwa klabu hizo mbili kukutana, mechi zote zikiwa katika Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya/Kombe la Ulaya.
Mchezaji Cristiano Ronaldo mpaka sasa amefunga jumla ya magoli 600
katika club alizowahi kucheza pamoja na timu ya taifa, ambapo katika kilabu ya
RealMadrid amefunga magoli 406, Manchester United amefunga
jumla ya magoli 118, huku katika timu yake ya taifa akifunga jumla ya magoli 71
na Sporting CP akifunga magoli 5.
0 comments:
Post a Comment