WANAUME WENYE UWARAZA HATARINI KUUAWA MSUMBIJI

Wanaume wenye uwaraza nchini Msumbiji wapo kwenye hatari ya kushambuliwa kutokana na kile kinachoaminika kuwa ni Imani za kishirikina zinazohusishwa na matambiko baada ya wanaume wawili wenye uwaraza nchini humo kuuawa mwezi uliopita.

Polisi nchini humo wametoa angalizo juu ya suala hilo kuwa pengine mauaji zaidi ya wanaume wenye uwaraza kutokana na imani za kishirikina yakatokea, hivyo jeshi la poliisi nchini humo limewaasa wanaume wenye uwaraza kuwa waangalifu.
Wanaume wawili hao ambao walikuwa na uwaraza waliuawa mwezi uliopita huku mmoja wao mwili wake ukipatakana ukiwa umekatwa kichwa huku baadhi  ya viungo vya mwili vikiwa vimetolewa, tukio hilo la mauaji ya wanaume hao  wawili lilitokea katika mkoa wa Zambezi nchini humo.
Msemaji wa jeshi la polisi Inacio Dina  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kusema mwezi uliopita mauaji ya wanaume wenye uwaraza yalisababisha kukamatwa kwa washukiwa waili wa tukio hilo.
 "Mwezi uliopita mauaji ya watu wawili wenye vipara yalisababisha kukamatwa kwa washukiwa wawili," msemaji wa polisi Inacio Dina, aliwaambia waandishi wa habari kwenye mkutano mjini Maputo
Hata hivyo washukiwa hao wawili waliliambia jeshi la polisi nchini humo kuwa viungo hivyo vilikuwa na lengo la kutumiwa kwenye uchawi na matambiko nchini humo nan chi jirani ya Tnzania.

Kufuatia kauli hiyo Tanzania inaendele kuwa miongoni mwa nchi zinazoamini na kuendeleza matumizi ya viungo vya binaadamu ambapo tayari viungo vya walemavu wa ngozi (Albino) vimekuwa vikitumika katika Imani hizo.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment