Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imezikana
pesa ambazo zilirudishwa na aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini Mhe. Wiliam
Mganga Ngeleja ikiwa ni sehemu ya mgawo wa ESCROW alioingiziwa kwenye akaunti
yake na mfanaybiashara James Rugemarira ambaye hivi sasa yupo rumande kwa
mashtaka ya ubadhirifu.
Waziri wa Nishati na Madini wa zamani
Ngeleja aliwasilisha TRA kiasi cha Shilingi za kitanzania Milioni 40.4 Jumatatu
iliyopita ambazo aliingiziwa kwenye akaunti yake huku akionesha nakala pamoja
na risiti za miamala hiyo ya fedha na visibitishi vingine kuwa amezirudisha
fedha hizo na ziko mikononi mwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).
Ngeleja alieleza sababu ya kurudisha fedha
hizo kuwa ni kujiondoa kwenye kashfa za ufisadi ambazo angeweza kushutumiwa
kutokana na kiasi hicho cha edha alichogawiwa na James Rugemarira bila ya kujua
kuwa ni mgawo wa ESCROW.
Ngeleja ambaye kwa sasa ni Mbunge wa
Sengerema (CCM) aligaiwa Sh. milioni 40.4 na mfanyabiashara maarufu James
Rugemalira ambaye mwanzoni mwa mwezi alifikishwa mahakamani akikabiliwa na
mashtaka 12, yakiwamo ya kughushi na utakatishaji fedha.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) imekana
kuwa hazitambui fedha hizo na kuwa, mamalaka hiyo ina jukumu la kukusanya
mapato pekee na si vinginevyo
Akizungumza
na Nipashe mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TRA, Richard
Kayombo alisema mamlaka hiyo inahusika na kuhakikisha serikali inakusanya kodi
stahiki na siyo urejeshaji wa fedha za kashfa kama Escrow.
Kayombo
alitoa ufafanuzi huo wakati alipoulizwa na Nipashe juu ya utaratibu rasmi
uliopo wa urejeshaji wa fedha hizo endapo wanufaika zaidi wa mgawo wa
Rugemalira watataka kufuata nyayo za Ngeleja.
Akifafanua
zaidi juu ya suala hilo, Kayombo alisema TRA haihusiki na fedha zilizochotwa
kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kwa kuwa hazikuwa mali yake.
Aidha,
Kayombo alisema TRA haiwezi kuzizungumzia fedha hizo kwa kuwa hazijawahi kuwa
mali yake na kuelekeza watafutwe wenye fedha hizo kwa ufafanuzi zaidi.
“Fedha
za Escrow zinaihusu vipi TRA? Tunawezaje kukaa na kuzungumzia fedha ambazo si
zetu?” Alisema Kayombo. “Mimi nashauri watafutwe wenyewe wazungumze kama
wanataka kurejesha… siyo sisi.”
0 comments:
Post a Comment