Kongamano lilodumu kwa siku mbili kwa
kuwakutanisha watanzania waishio Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference)
limehitimishwa hii leo Agosti 24, 2017 huku likiwa limehudhuriwa na Diaspora
350 na kuchagizwa na wahudhuriaji wengine ambao ni watendaji kutoka taasisi za
serikali na wadau katika uwekezaji na uchumi.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy |
Kongamano la nne la Watanzania waishio
ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) lilifunguliwa jana tarehe 4 Agosti
2017 na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB) alipomuwakilisha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan
ambapo limefikia ukomo kwa kupatikana majibu ya changamoto mbalimbali
ziwahusuzo Diaspora ikiwemo uraia pacha na sera ya utambuzi wao nchini
Tanzania.
Akihutubia mamia ya watanzania walioshiriki
katika hafla ya chakula cha jioni iliyojulikana kama Swahili Barbeque Night
iliyofanyika mji Mkongwe katika ukumbi wa Ngome kongwe-Zanzibara, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd alisema
kuwa serikali inawatambua Diaspora kama mabalozi muhimu katika kutangaza utalii
Duniani kote jambo ambalo kwa kiasi kikubwa linaongeza kipato cha nchi.
Alisema kuwa serikali inatambua kazi kubwa
inayofanywa na Diaspora katika kuitangaza nchi ya Tanzania na vivutio vyake
hivyo kuwataka kutumia fursa hiyo pia kuwatangaza viongozi wa serikali kwa
weledi mpana pasipo kueneza chuki dhidi ya viongozi wao.
Mhe alozi Seif alisema kuwa kumekuwa na
watanzania waishio nje ya nchi wasiokuwa na weledi na nidhamu dhidi ya viongozi
wa serikali kwani wamekuwa wakiwasema vibaya kwa kuwatukana na kejeli jambo
ambalo linarudisha nyuma heshima yao waliyonayo na kutia doa serikali.
Alisema kuwa Diaspora wanapaswa kuendelea
kushiriki katika makongamano mengine yajayo kwani kufanya hivyoi kunatoa fursa
kwao kuishauri serikali na kuona namna bora ya utambuzi wao.
Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira
wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku
akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida
itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla
wake.
Alisema kuwa ushirikiano huo wa Diaspora
kupitia makongamano yote yaliyopita umeimarisha zaidi mahusiano chanya bila
kujali dini wala kabila jambo ambalo limeongeza utu, umoja na mshikamano.
Mhe alozi Seif alisema kuwa Diaspora
wanatakiwa kuheshimu sheria, taratibu na taratibu za nchi wanazoishi ili kue
delea kuipatia sifa chanya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Naomba nikukumbusheni nyote mliohudhuria hapa
hii leo kutamnbua kuwa mchumia juani hulia kivulini nanyi kivulini kwenu ni
hapa nyumbani hivyo tumie fursa ya uwekezaji vizuri huku mkikumbuka kuwa mkataa
kwao ni mtumwa zaidi endelezeni umoja na mshikamano kwani inafahamika kuwa
umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.” Alisema Balozi Seif Ally Idd
Kongamano la nne la watanzania waishio
ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) linaratibiwa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kusudio la kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna
ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano kama hilo linaakisi makongamano
matatu ya utangulizi yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam huku
kongamano la mwaka 2016 na mwaka huu 2017 yakifanyika visiwani Zanzibar huku
likiwa limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini
ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”
Kongamano la watanzania waishio ughaibuni kwa
mwaka 2017 limedhaminiwa na PBZ Bank, ZSSF, Idara ya Uhamiaji, Sea Cliff Hotel,
CRDB Bank, Mult Colour, Equity Bank, Zanzibar Cable Television, ZBS, Watumishi
Housing Cooparation na Petro.
0 comments:
Post a Comment