Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa vifaa vipya kwa ajili ya vyumba
viwili vya upasuaji wa watoto wenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5 kutoka Taasisi
binafsi ya Archie Wood Foundation ya Scotland ili kufanya huduma hiyo kupatikana
kwa urahisi nchini.
Akizungumza
katika uzinduzi wa vyumba vya upasuaji kwa watoto uliofanyika leo jijini Dar es
salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
amesema kuwa msaada huo umeonyesha jinsi gani Wahisani wana ushirikiano na Serikali
katika kuleta maendeleo hasa katika sekta ya afya nchini.
“Kutokana
na Wahisani kujitokeza mara kwa mara katika kushirikiana na Serikali yetu kwenye
sekta ya afya tumepunguza asilimia 40 ya
wagonjwa wanaokwenda nje kwa ajili ya matibabu na lengo letu ni kupunguza asilimia
70 mpaka kufikia 2025” alisema Waziri
Ummy.
Aidha
Waziri Ummy ameongeza kuwa Wazazi na walezi wawe mstari wa mbele kuwakatia watoto
wao bima ya afya ijulikanayo kama Toto Afya kwa gharama ya shilingi elfu 54 ili
kuokoa gharama zingine zisizo na lazima kwa ajili ya kupata matibabu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Laurence Museru amesema kuwa kutokana
na msaada wa vifaa hivyo Hosiptali hiyo inatimiza idadi ya vyumba viwili vya upasuaji
vilivyokamilika kwa ajili ya upasuaji wa watoto.
“Tulikua
tunafanya upasuaji kwa watoto wadogo mara tatu kwa wiki kutokana na ufinyu wa vifaa
lakini kutokana na vifaa hivi tutafanikiwa kufanya upasuaji mara kumi kwa wiki”
alisema Prof. Museru.
0 comments:
Post a Comment