NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI MHE SULEIMAN SAID JAFO ATEMBELEA JIMBO LA CHALINZE


Naibu waziri wa TAMISEMI (Tawala za mikoa na serikali za mitaa) Mhe. Suleiman Jafo ametembelea wilaya ya Bagamoyo na kuzungumza na wadau wa maendeleo wa wilaya hiyo ikiwemo mbunge wa jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete, pia alipata nafasi ya kuona ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, ujenzi wa bwalo, maabara za masomo ya sayansi na hosteli ambazo zitachukua wanafunzi 796 katika shule ya sekondari Mboga ambazo zitawasaidia wanafunzi wa shule hiyo hususani wasichana na adha ya vishawishi na kutembeo mwendo mrefu. 


Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI wa tatu kutoka kushoto akiongozana na mbumbe wa jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete kwenye kikao cha kuzungumza na wadau wa maendeleo na watumishi wa halmashauri.

Mbubge wa Chalinze akieleza machache kabla hajamkaribisha mheshimiwa naibu waziri azungumze katika kikao hiko.

Mheshimiwa Naibu Waziri Suleiman Jaffo alipata nafasi ya kutembelea shule ya Sekondari ya Mboga ambayo iko katika ujenzi. Alitazama ujenzi wa Maabara tatu za masomo ya sayansi zinazojengwa, ujenzi wa madarasa mawili, jiko la kisasa, bwalo na hostel ambazo zitachukua wanafunzi  796. 
Mheshimiwa Mbunge wa Chalinze akitoa maelezo juu ya ujenzi wa hostel unaoendelea kwa mheshimiwa naibu waziri. 

 Diwani wa kata ya Msoga na Mbunge wa Chalinze wakifurahi jambo na mgeni wao.

Naibu waziri Jaffo akiwa na wenyeji wake kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Alhaj Majid Mwanga, mkurugenzi wa Halmashauri Ndg. Zikatimu na Mhehimiwa mbunge walipokwenda kagua shule ya Sekondari ya Mboga.
Dada mkuu wa shule ya sekondari ya Mboga akizungumza neno kumshukuru Mbunge kwa msaada wa ujenzi wa Hostel na kukamilisha Maabara na kumuahidi kuwa watasoma kwa bidii ili asife moyo kusaidia elimu.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment