Rais mpya wa nchi ya Somalia Abdullahi Mohamed, ametangaza kuwepo kwa baa la njaa katika nchi yake, umoja wa mataifa umesema idadi inayokadiriwa kuhitaji msaada nchini humo ni nusu ya idadi ya watu milioni 10.
Hii inatokea siku chache tu baada ya hali hiyo kutangazwa kuwepo katika nchi ya Kenya.
Rais Abdullahi Mohamed siku ya jumanne alitangaza rasmi kuwepo kwa baa la njaa nchini kwake, katika mkutano uliofanyika mjni Mogadishu kwa kudhaminiwa na umoja wa mataifa, alisema "Hatuwezi na hatulazimiki kusubiri" kuomba misaada kutoka katika mashirika ya misaada, akizungumza katika mkutano huo alisema jumuiya za wafanyabiashara wa Somalia walioko duniani kote wanatakiwa kusaidia kuondokana na baa hilo.
Katika wiki za karibuni wanawake kadhaa walionekana wakiwa wamebeba watoto wenye afya dhoofu katika mjii mkuu wa nchi hiyo kuomba msaada wa chakula.
Hata hivyo umoja wa mataifa umeonya ya kwamba kutokuwepo kwa maji salama katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo ni tishio la kutokea kwa magonjwa ya mlipuko hususani kipindipindu.
0 comments:
Post a Comment