Mwanamume mmoja raia wa Marekani
ambaye alimfunga mbwa wake kwenye mdomo, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano
jela.
William Dodson, mwenye umri wa miaka 43, anasema alimfunga mbwa
huyo mdomoni kwa sababu alibweka sana. Ililazimu mbwa huyo kufanyiwa upasuaji
mara kadha baada ya kupoteza sehemu ya ulimi wake.
Siku moja baada ya hukumu hiyo kutolewa, William Dodson pia
alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela, kwa mashtaka tofauti ya bunduki. Ambapo vifungo
hivyo vyote viwili vitafuatana.
Kulingana na polisi William Dodson alimnunua mbwa hiyo kwa jina
Caitlyn kwa dola 20. Dodson, ambaye alikuwa huru kwa dhamana wakati huo,
alimfunga mbwa huyo nje baada ya kumfunga mdomo wake mara tisa.
Lakini mbwa huyo alifanikiwa kutoroka mwezi Mei mwaka 2015, na
alikuwa mgonjwa sana wakati alipatikana akirandaranda barabarani. Hata hivyo
kamba aliyotumia kumfunga mbwa huyo ilizuia damu kufika hadi kwenye ulimi wake,
na iliwachukua madaktari wa mifugo karibu saa 36 kuiondoa.
Wakati huo chama cha wanyama cha Charleston, kibadilisha picha
ya akaunti yake na kuweka picha ya mbwa huyo, kama njia ya kuonesha uzalendo.
Wamekuwa wakichapisha taarifa jinsi mbwa huyo anavyoendelea
katika kisa hicho kilichoangaziwa kimataifa. Caitlyn, alikuwa na umri wa miezi
15 wakati alipatikana na sasa amehitimu miaka mitano akiwa anaishi na familia
tofauti.
0 comments:
Post a Comment