PARK GUENI |
Alipoteza kinga ya rais dhidi
ya kfuunguliwa mashtaka mapema mwezi huu na akaondolewa rasmi madarakani baada
ya mahakama ya kikatiba kudumisha uamuzi wa bunge wa kumng'oa madarakani.
Bi Park anatuhumiwa kumruhusu
rafiki yake wa karibu Choi Soon-sil kudai pesa kwa lazima kutoka kwa kampuni
kubwakubwa hata hivyo Bi Park amekanusha madai hayo.
BI CHOI SOON ALIYEVALI NYEUPE |
Rais huyo wa zamani aliomba radhi kwa umma wiki iliyopita, kabla
ya kuhojiwa na maafisa wa mashtaka kwa saa 14. Waendesha mashtaka walisema
Jumatatu kwamba "wameamua kwamba ni vyema, kwa kufuata sheria na maadili
nchini humo, kuomba kibali cha kumkamata".
Wanasema ushahidi, ambao unapatikana katika diski za kompyuta
huenda ukaharibiwa iwapo Bi Park hatakamatwa. Bi Choi amefunguliwa mashtaka ya
ulaji rushwa na tayari kesi dhidi yake imeanza. Bi Park aliondolewa madarakani
kutokana na uhusiano wake wa karibu na Bi Choi.
Bi Choi anatuhumiwa kutumia uhusiano wake na rais huyo
kushinikiza kampuni kutoa mamilioni ya dola kama mchango kwa nyakfu za kusaidia
jamii ambazo alikuwa anazisimamia.
Kaimu mkuu wa kampuni kubwa ya
vifaa vya kielektroniki ya Samsung, Lee Jae-yong, alikamatwa kuhusiana na
kashfa hiyo.
Bi Park, 65, anadaiwa kuhusika
moja kwa moja katika hili, na kwamba alimruhusu Bi Choi uhuru wa kiwango
kisichokubalika wa kufikia nyaraka rasmi za serikali.
0 comments:
Post a Comment