MWAKYEMBE AAMURU NEY WA MITEGO AACHIWA HURU

Waziri wa Habari nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe ameagiza msanii aliyekamatwa kuhusiana na wimbo wake alioutoa hivi karibuni aachiliwe huru.
Sehemu ya maudhui ya wimbo huo inagusia tuhuma za kughushi vyeti ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari nchini Tanzania
Nay wa Mitego hata hivyo ametakiwa auboreshe zaidi wimbo wake, kwa mujibu wa ujumbe uliopakiwa katika ukurasa Rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania kwenye Twitter.
Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali
Waziri Mwakyembe alizungumza na Rais Magufuli juu ya suala hilo na rais Magufuli alimtaka Mwakyembe aamuru kuachiwa huru kwa msanii huyo na kwamba wimbo huo auboreshe zaidi.
“Nimeongea na Rais akatoa ushauri huo wimbo wa 'WAPO' auoboreshe uwe mzuri zaidi wala asiondoe chochote” alisema Mwakyembe


Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment